(-5.0062273, 36.1323458) KAGAME: TUMEONDOA VIZA KWA AFRIKA - Uniprofits Media

Uniprofits Media

Get updated on daily news. All about politics, economics, education, sports and games and other trending news.

Breaking

Post Top Ad

/div>

Translate

2023/11/04

KAGAME: TUMEONDOA VIZA KWA AFRIKA

Na uniprofits Media 







RWANDA: Siku chache baada ya Rais William Ruto kutangaza kuwa Kenya itafuta ulazima wa Raia wa Nchi zote za Afrika kuingia nchini humo kwa Viza. Kufikia mwishoni mwa mwaka 2023, Rais Paul Kagame wa Rwanda ametangaza kuwa Raia wa Nchi zote za Afrika hawahitaji tena kuwa na Viza kuingia Rwanda.
Kwa mujibu wa Kagame, kigezo cha Viza kimekuwa kikwazo kwa maendeleo ikiwemo kupunguza idadi ya Watalii wakati Bara la Afrika ndio kituo kikuu cha Utalii Duniani. Hivyo, nchi za Afrika zinazondelea kutumia kigezo hicho zinajikwamisha zenyewe.
Rwanda inakuwa Nchi ya 4 Afrika kufuta kigezo cha Viza. Nchi nyingine ni Benin, Ushelisheli na Gambia. Kenya itakuwa Nchi ya 5 kama itatekeleza ahadi yake ifikapo mwishoni mwa mwaka 2023.
Na uniprofits Media
Follow us +

No comments:

Post Top Ad

Your Ad Spot

FOLLOW US