Picha
TAZAMA/SIKILIZA VIDEO
BUNGENI: Mbunge wa Tarime vijijini, Mwita Waitara akichangia mjadala wa ripoti ya CAG, amesema watumishi wanaobainika kuiba fedha za Umma waanze Kunyongwa kwasababu watanzania wengi wanaishi maisha ya ufukara kiasi cha kushindwa kuwalipia ada watoto kutokana na ubadhirifu huo.
Amesema suala hilo linafanyiwa uzembe na wabunge kwa kutochukua hatua na kuongeza "Kama mtu amebainika ameiba na ripoti ipo, taarifa zipo, vyombo vipo, lakini hawajibishwi, je, wanafundisha nini vijana wa Tanzania? Kwamba mtu ataiba na kuhamishwa tu Wizara bila ya kuwajibika?"
Waitara amesema Wabunge wasisubiri kuambiwa wanatakiwa kuchukua hatua, bali wawawajibishe watumishi wanaotajwa katika ripoti hizo kwasababu wao ndio wenye dhamana ya kufanya hivyo.
Na Uniprofits Media

No comments:
Post a Comment