Akizungumza zaidi, Msanii Black Rhyno ambaye ni mdogo wa Prof. Jay amesema kuna wakati kaka yake alipata hali ya Moyo kusimama mara 3 katika vipindi tofauti lakini juhudi za Madaktari na huruma ya Mungu zilimnusuru na kifo mkongwe huyo.
Aidha, Prof. Jay akizungumza na Clouds FM amesema Ugonjwa huo ulimlazimu kuchoma Sindano 10 zilizogharimu Tsh. Milioni 50 na baadaye alipelekwa Hospitali iliyopo India, na hilo limemsukuma kuanzisha 'Foundation' itakayohusika na masuala ya kusaidia Wagonjwa wa Figo.
Fuata/follow Uniprofits Media hapo chini.

No comments:
Post a Comment